KATIBU WA CHAMA CHA ACT WAZALENDO NDEMBEZI BWANA STANSLAUS BUKUKU AJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAKAZI

Katibu wa Chama cha ACT Wazalendo kata ya Ndembezi, Bw. Stanslaus S. Bukulu, amejiandikisha katika daftari la mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
 
 Baada ya kujiandikisha ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha wananchi kujiandikisha ili kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo ujao wa serikali za mitaa.

 Bw. Bukulu amesisitiza umuhimu wa wananchi kuchukua hatua hiyo mapema ili kupata haki yao ya kuchagua viongozi watakaowakilisha maslahi yao. 

Ameendelea kutoa wito kwa wakazi wa Ndembezi kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo.

Previous Post Next Post