MATOKEO YA KURA ZA MAONI MTAA WA VIWANDANI, MJINI KUPITIA CCM ASHRAF MAJALIWA ASHINDA TENA

Katika uchaguzi wa kura za maoni uliofanyika jana Oktoba 23, 2024 katika mtaa wa Viwandani, kata ya Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), matokeo yameonyesha ushindi mkubwa kwa Ashraf Majaliwa.

Ashraf Majaliwa ameibuka mshindi kwa kupata kura 88, akiwashinda wapinzani wake kwa tofauti kubwa. Suleiman Abedi alishika nafasi ya pili kwa kura 31, akifuatiwa na Louis Kwiyukwa aliyepata kura 04, na Michael Saliga aliyepata kura 03.

Uchaguzi huo ni sehemu ya mchakato wa kupata mgombea atakayewakilisha CCM kwenye uchaguzi wa mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27.

Tukio hilo limefanyika kwa amani, huku wajumbe wakionesha nia ya dhati ya kuimarisha demokrasia ndani ya chama.



Previous Post Next Post