MNEC JOYCE MANG'O AMTUA MAMA NA MWANAFUNZI NDOO KICHWANI NYAMWAGA TARIME.



Na Gabon Mariba, Mara.

Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa Ndg.Joyce Ryoba Mang'o ambaye amekua Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Kidato cha nne shule ja Sekondari JK Nyerere iliyopo Kata ya Nyamwaga Tarime Vijijini Mkoani Mara, ambapo ameahidi kupatikana kisima chenye thamani zaidi ya Milion 20, kitakacho ondoa adha ya wanafunzi wa wakazi wanaozunguka mazingira ya shule hiyo.

Akizungumza wakati wa kujibu Risala Ndg.Joyce amewapongeza wahitimu kwa uvumilivu na kuwataka kutia bidii katika masomo ili kupata ufauru wanapoelekea kufanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne.

Aidha amesababisha kupatikana zaidi ya Tsh.1.2M kwaajili ya chakula cha wanafunzi, Mchele Kg 200 na Ng'ombe 1 pindi watakapokuwa kwenye mitihani.

Ameendelea kuwapongeza viongozi wa chama na serikali kwa ushirikiano haswa wabunge, Madiwani na Waalimu katika kuhakikisha miundombinu na Upatikanaji elimu inawafikia wanafunzi inavyotakiwa.

Pia ameahidi ushirikiano wa kimaendeleo wakati wowote watakapo hitaji msaada kwaajili ya kusapoti na kuunga Juhudi za Mhe.Rais Dk.Samia Suluh Hassan.


 


Previous Post Next Post