Ticker

6/recent/ticker-posts

MWENYEKITI WA CCM SHINYANGA MJINI MHE. ANORD MAKOMBE ATOA WITO KWA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAKAZI

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anord Makombe, amewahimiza wakazi wa Manispaa ya Shinyanga kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wakazi ili kuwa na haki ya kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Makombe ametoa wito huo baada ya kujiandikisha mwenyewe katika daftari hilo katika Mtaa wa Bushushu, Kata ya Lubaga, ambapo ametumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.

Ameeleza kuwa ni muhimu kwa kila mwananchi mwenye sifa kujiandikisha ili kupata nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi ujao.

Wakizungumza na Misalaba Media baadhi ya wakazi wa Bushushu, Kata ya Lubaga, wamekiri kuwa tayari wameshajiandikisha ambapo wametoa wito kwa wenzao kujitokeza kwa wingi kabla ya muda wa zoezi hilo kumalizika.

Zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wakazi limeanza Oktoba 11 na linatarajiwa kumalizika Oktoba 20, 2024, huku uchaguzi wa serikali za mitaa ukitarajiwa kufanyika Novemba 27, Mwaka huu 2024.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anord Makombe akielekea katika kituo cha kujiandikisha.




 

Post a Comment

0 Comments