MKURUGENZI WA MANISPAA YA SHINYANGA MWL. KAGUNZE AITAKA KAMATI YA LISHE KUSIMAMIA KILIMO CHA MBOGAMBOGA NA MATUNDA KWENYE SHULE ZOTE ZA MSINGI NA SEKONDARI

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze ameitaka kamati ya Lishe kushirikiana na maafisa kilimo kata pamoja na maafisa elimu sekondari na msingi kuhamasisha shule zote za sekondari na Msingi zenye maeneo kulima mbogamboga na miti ya matunda ili kujenga afya bora kwa wanafunzi.

Mkurugenzi Kagunze ametoa maelekezo haya leo Oktoba 25,2024 wakati akizungumza kwenye kikao Cha kwanza Cha robo ya kamati ya lishe 2024/2025.

“Tunamaafisa kilimo kila kata zetu,sasa nendeni mkashirikiane na maafisa Elimu sekondari na Msingi kuwahamasisha waalimu kusimama kilimo Cha mbogamboga na matunda haswa msimu huu wa mvua zinaanza kunyesha”.Amesema Mwl. Kagunze.

Kwa upande wake afisa Lishe Manispaa ya Shinyanga Ndg.Amani Mwakipesile akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi kwenye kikao hicho amesema Jumla ya kinamama wajawazito 9388 kati ya 9487 sawa na asilimia 98.9% wamefanikiwa kupewa dawa za kuongeza Damu ili kuzuia vifo vya wajawazito (Dawa aina ya FEFO) kwa kipindi husika.

















 

Previous Post Next Post