ASKOFU SANGU ATOA WITO KWA WATANZANIA KUOMBA AMANI YA TAIFA HASA KUELEKEA KATIKA KIPINDI CHA UCHAGUZI


Askofu Sangu amesema kushiriki mchakato wa Uchaguzi ni haki ya msingi ya kila mtanzania, lakini ni muhimu kusali na kuomba kwa ajili ya Amani ya Nchi ili kufanikisha mchakato huo.
Amesisitiza zaidi kuendelea kuiombea Tanzania ili iendelee kustawi katika haki,Amani umoja na mshikamano.
"Katika kipindi hiki tuliombee taifa letu na hasa tunapoelekea kwenye chaguzi zijazouchaguzo uwe wa Amani,Umoja na Mshikamano tuongozwe na Mungu roho Mtakatifu katika kufanya zoezi hili ni haki yetu na ni haki ya Kila mmoja wetu tuliombee nchi yetu uendelee kustawi katika Hali,Amani Umoja na Mshikamano"
Katika mahubiri yake Askofu Sangu ameonya waumini wa kanisa hilo wenye dhamana ya kutoa huduma za kijamii katika taasisi mbalimbali, kwamba wasitumie shida na matatizo ya watu wenye uhitaji kama fursa ya kujinufaisha,na badala yake wanapaswa kuwa chimbuko la faraja kwa wengine.
Katika ziara yake ya kichungaji katika parokia ya Maganzo, Askofu Sangu ameongoza misa takatifu katika kanisa la mtakatifu Yohane wa 23, ambapo ametoa sakramenti ya kipaimara kwa waumini 30.

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA PAROKIA YA MTAKATIFU YOHANNE WA 23 MAGANZO WAKATI WA ADHIMISHO LA MISA TAKATIFU YA KIPAIMARA ILIYOONGOZWA NA ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI SHINYANGA MHASHAMU LIBERATUS SANGU.

 

Previous Post Next Post