Na Elisha Petro, Misalaba Media
Klabu ya Stand United (chama la wana) yenye makazi yake Mkoani Shinyanga imezindua jezi zake mpya zitakazotumika msimu wa 2024/2025 katika michezo mbalimbali ikiwemo ligi ya NBC Championship ambapo kila jezi itauzwa kwa Tsh 25000.
Hafla ya uzinduzi wa jezi hizo imefanyika katika uwanja wa Zimamoto (fire) uliyopo Nguzo nane Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga.
Baada ya hafla hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindo na Usajili wa Stand United Chrispin Kakwaiya amewaomba wanachama na mashabiki wa timu hiyo kujitoa kwa mawazo,maneno na vitendo ili kufanikisha kuipandisha timu hiyo ndani ya ligi kuu msimu ujao.
"Mashabiki wote wa Stand United kutoka Stand zote Tanzania lazima tuungane chimbuko la timu hii ni Stand yaani Stand yoyote ile iwe ya mabasi,pikipiki hata baiskeli hii ni timu ya Kila mmoja wetu kurejea ligi kuu kunahitaji sana ushirikiano jambo pekee,Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa Wilaya hawawezui kufanikisha timu kurejea ligi kuu tunahitaji kuwa na ushirikiano uwe mfanyabiashara au mtumiaji wa Stand yoyote Tanzania wote tunapaswa kuungana pamoja na kuisaidia timu yetu kwa mawazo,maneno na zaidi kwa vitendo"
Wakati huohuo Afisa habari wa timu ya Stand United Bwana Ramadhani Zolo amewasisitiza mashabiki kujitokeza kwa wingi kununua jezi hizo zilizo na ujumbe wa kuwaunganisha mashabiki wa timu hiyo ndani na nje nchi.
"Ujumbe ambao umebebwa na hizi jezi ni muungano wa sisi Stand United chama la wana kwa ajili ya kurudi tena ligi kuu Tanzania bara hizo rangi zote zilizopo kwenye jezi ndiyo rangi za klabu yetu ikiwemo Orange,nyeupe na Blue huu ni ubunifu ambao tumeufanya kuhakikisha jezi yetu inakua kali mahali popote ulipo unaweza kupata jezi yako kwa hapa Shinyanga duka lolote lenye vifaa vya michezo unaweza kupata jezi yako lakini pia hizi jezi zitakuwa zinatembezwa kwenye michezo yetu tutakapokuwa tunacheza na huko pia unaweza kujipatia jezi yako kwa urahisi"
Kwa upande wake kocha Mkuu wa timu hiyo Abdul Mingange ameupingeza uongozi wa Kampuni ya Jambo kwa utayari wa kuisaidia timu hiyo na kuwaomba wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuendelea kumuunga mkono mdhamini kutimiza ndoto na malengo ya kupanda ligi kuu msimu ujao.
"Matatizo ya timu za championship Kila mtu anafahamu lakini niseme ukweli Kampuni ya Jambo wanajitahidi sana kwa kadri ya uwezo wao kuisaidia timu, Mimi nimeshakaa kwenye hizi timu najua lakini naweza kuwaambia kwamba wanachama na mashabiki wote wawaunge mkono jambo ili tutimize ndoto ya kupanda ligi kuu msimu ujao kuemdesha timu ni gharama kwa hiyo kumuachia tu mdhamini anayetufadhiri ni mzigo mkubwa kwa hiyo wawe karibu mwenye mbili tatu asaidia na tukiuachia uongozi wa serikali peke yake haziwezi kutosha kusaidia wanachama na mashabiki wenye nia njema wasaidia timu tupande ligi kuu"
Kesho jumapili ya tarehe 20.10.2024 Stand United itashuka Dimbani kuwakaribisha wageni wao Bigman FC majira ya saa 10:00 jioni uwanja wa CCM Kambaraga.