RODRI MSHINDI WA TUZO YA BALLON D'OR 2024, AINGIA KWENYE VITABU VYA MANCHESTER CITY.


Kiungo wa timu ya Manchester City Rodrigo Hernandez Cascante mefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2024 Duniani (Ballon d’Or 2024) na kuwashinda wachezaji 30 waliochaguliwa kuwania tuzo hiyo akiwemo Vin Junior,Jude Bellingham, Harry Kane na wengine wengi.

Rodri ameisaidia timu yake ya taifa ya Hispania kutwaa ubingwa wa Euro 2024  akiisaidia timu yake kutwaa ubingwa huo baada ya mwaka 2012.

Amecheza michezo 63, amefunga mabao 12. Ametoa pasi za mwisho za magoli 14. Makombe aliyobeba ni Ligi Kuu England, Uefa Super Cup, Klabu Bingwa Dunia na Euro 2024.

Rodri anakuwa mchezaji wa kwanza wa Manchester City kushinda  kushinda tuzo hiyo ya BALLON D'OR.

Tuzo zingine zilizotolewa usiku wa Ballon D'OR ni tuzo ya klabu bora ya mwaka 2024 iliyoenda kwa Real Madrid, tuzo ya kocha bora wa mwaka iliyoenda kwa  Carlo Ancellot kocha mkuu wa Real Madrid, tuzo ya golikipa bora aliyoinyakuwa golikipa wa Aston Villa na timu ya taifa ya Argentina Emiliano Martinez na ametwaa mara mbili mfululizo mwaka 2023 na mwaka 2024.

Wengine ni Lamine Yamal nyota wa klabu ya FC Barcelona aliyenyakua tuzo ya mchezaji bora kijana wa mwaka 2024, Harry Kane  na Kylian Mbappe wametwaa tuzo ya mshambuliaji bora wa mwaka kwa kufanikiwa kufunga magoli 52 Kila mmoja kwa msimu wa 2023/2024.

Klabu ya FC Barcelona ya wanawake imefanikiwa kutwaa tuzo ya klabu bora ya wanawake kwa mwaka 2024 huku nyota wa kikosi hicho Aitana Bonmati akitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka (Ballon D'OR 2024) na kufanikiwa kuitetea tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo.

Previous Post Next Post