Mary Makamba akizungumza na Misalaba Media baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya mwenyekiti mtaa wa Bugweto A kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Mary Makamba amechukua fomu rasmi ya kugombea nafasi
ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugweto A, kata ya Ibadakuli, Manispaa ya Shinyanga,
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hatua hiyo inampa nafasi ya kuendelea kuwawakilisha
wananchi wa mtaa huo kwa awamu ya tatu.
Akizungumza na Misalaba Media, Makamba ametoa
shukrani zake kwa wananchi kwa kuendelea kumwamini kupitia CCM, akiahidi
kuendelea kushughulikia changamoto zinazowakabili.
"Nimechukua fomu leo katika ofisi ya
mtendaji wa Bugweto A, na tunatarajia kurudisha kesho mimi na wajumbe wangu
tunawaomba wananchi waendelee kutuamini; tutashughulikia changamoto zilizopo
kwa kuzingatia ilani ya CCM," amesema Makamba.
Makamba ameonesha furaha yake kwa imani ambayo
wananchi wamempa, akieleza kuwa uzoefu alionao utamsaidia kutimiza wajibu wake baada
ya kupata ufanisi ya kuwa Mwenyekiti wa
mtaa.
"Nawashukuru
sana wananchi wa Bugweto A kwa kuniamini tena kwa awamu ya tatu mungu ni mwema,
na si mara yangu ya kwanza kufanya kazi hii uzoefu wangu ni faida kwa mtaa
wetu, na yote haya ni mapenzi ya Mungu," amesema Makamba.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika
Novemba 27, 2024, ambapo wananchi watapata nafasi ya kuchagua viongozi wao wa
mitaa, vijiji, vitongoji, na wajumbe wao.
Mary Makamba akizungumza na Misalaba Media baada ya
kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya mwenyekiti mtaa wa Bugweto A kupitia tiketi
ya chama cha mapinduzi CCM.
Mary Makamba akizungumza na Misalaba Media baada ya
kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya mwenyekiti mtaa wa Bugweto A kupitia tiketi
ya chama cha mapinduzi CCM.
Burudani ikiendelea.