CHADEMA WAPINGA TAARIFA ZA KUJIWEKA KANDO NA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024


 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekanusha vikali taarifa zinazozagaa mitandaoni kuwa chama hicho kimejiondoa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024. Katika taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho, John Mrema, Chadema imeelezea kwamba taarifa hizo ni za uzushi na zinapaswa kupuuzwa.

Aidha, Chadema imesisitiza kuwa hawana mpango wowote wa kujiondoa kwenye uchaguzi huo kwa sasa. Mrema aliwahimiza wanachama wote waliochaguliwa katika maeneo mbalimbali nchini kujitokeza mapema kesho, Oktoba 26, 2024, kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali kupitia chama hicho.

Taarifa hiyo imetolewa huku kukiwa na msisimko wa maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambao ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.


Previous Post Next Post