Na Elisha Shambiti, Misalaba Media
Meneja wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kanda ya ziwa mhandisi
Imelda Salum amewataka watu wenye mahitaji maalum mkoani Shinyanga kutunza faragha zao binafsi pindi wanapotumia mitandao ya kijamii.
Ameyasema hayo leo katika ukumbi wa empire hoteli mjini shinyanga alipokuwa
akitoa elimu ya usalama mitandaoni yenye lengo la kuwajengea uelewa wa pamoja watu wenye mahitaji maalumu kwa kuwafundisha matumizi sahihi ya mtandao.
Mhandisi Imelda amesema kuwa baadhi ya watu wamekuwa na utamaduni wa
kuweka kwenye mitandao ya kijamii kila wanachokifaya pamoja na faragha zao
jambo ambalo linaweza kunahatarisha usalama wao na mali zao kwani taarifa hizo zinaweza kutumiwa na watu wenye nia ovu.
Mhandisi Imelda ameongeza kuwa jamii inapaswa kuwasiliana na watoa huduma
za mitandao ya simu kwa namba zao ramsi ambapo mitandao yote hutumia namba 100 kufanya mawasiliani na wateja wao na si namba za kawaida za kupiga simu ili kuepuka kutapeliwa.
Mamlaka ya mawasiliano kanda ya ziwa lmetumia nafasi kujibu maswali mbali mbali yaliyoulizwa na watu wenye mahitaji maaalum.