UONGOZI ENDELEVU WA SHULE KUJADILIWA MWANZA, MGENI RASMI MR. BLACK

Mkutano mkubwa wa uongozi wa shule unatarajiwa kufanyika leo tarehe 25 Oktoba 2024 katika ukumbi wa Shule ya Ziwa, Mwanza, ukiwaleta pamoja viongozi wa shule kujadili usimamizi bora wa shule, ushirikiano, na uendelevu wa kifedha.

Mgeni rasmi katika mkutano huo ni Peter Frank (Mr. Black) ambaye ni Mkurugenzi wa BSL Investment Company Limited, The True Life Foundation, na Shule za BSL. Mkutano huu unaandaliwa kwa ushirikiano na mashirika kama Elimu Connect, Edify, na TAPIE, ukilenga kutoa mbinu na mikakati ya kuhakikisha shule zinaendelea kuwa na uongozi thabiti na rasilimali endelevu.

Mkutano huo umeanza saa 2:00 asubuhi na utamalizika saa 7:00 mchana.
Previous Post Next Post