Ticker

6/recent/ticker-posts

VIJANA NA WANAWAKE WATAJWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO YA SERIKALI, ZIARA YA JUMUIYA YA WAZAZI CCM MNEC HAMOUD ASISITIZA AMANI NA MSHIKAMANO WAKATI WA UCHAGUZI

Na Mapuli Kitina Misalaba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Mhe. Hamoud Abuu Jumaa, amewataka viongozi na wanachama wa CCM kudumisha umoja na kuachana na makundi yenye nia mbaya, hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Mungula kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Mhe. Hamoud amesema wakati wa chaguzi makundi yenye mgawanyiko hujitokeza, jambo linaloweza kuvuruga mshikamano na kwamba amehimiza umuhimu wa kuendeleza umoja uliopo ili nchi ipite kwa amani katika chaguzi zijazo.

Vilevile, amewakumbusha wananchi kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu wa 2024, pamoja na uchaguzi mkuu ujao, huku akiwataka kuhakikisha wanachagua viongozi bora.

Pia, Mhe. Hamoud pamoja na mambo mengine amehimiza makundi ya vijana, wanawake, na watu wenye ulemavu kuchangamkia fursa za mikopo ya serikali ili kuinua uchumi wao.

Baadhi ya wakazi wa Kata ya Mungula na Malunga wameahidi kuendelea kuunga mkono serikali na kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi yao, huku wakiahidi kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuleta maendeleo.

Ziara ya Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa inaendelea mkoani Shinyanga, ambapo leo viongozi hao wametembelea na kuzungumza na wakazi wa Kata ya Mungula na Malunga, Manispaa ya Kahama.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) maarufu kama Mzee wa Sambusa Mhe. Hamoud Abuu Jumaa na viongozi wengine wakikagua vifaa vya ufyatuaji tofali kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya rufaa ya Wilaya ya Kahama ambavyo vimegharimu zaidi ya Milioni 30 na kwamba ni sehemu ya mradi wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Shinyanga.

Post a Comment

0 Comments