WAKAZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA WAASWA KUTUMIA FURSA YA UJIO WA MADAKTARI BINGWA KUPATA MATIBABU

Hayo yameelezwa na Dkt. Charles Zakaria kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakati akizungumzia ujio wa madaktari bingwa wa magonjwa ya akina mama na watoto ambao  wameanza kutoa huduma za kibingwa hospitalini hapo kuanzia Oktoba 14 2024 na huduma hizo zitatamatika Oktoba 18, 2024.

Akielezea kuhusu huduma za kibingwa zinazotolewa hospitalini hapo, Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Dkt. Mwita Chacha amesema lengo la kutoa huduma hizo ni kuwapunguzia wananchi  changamoto ya kutembea umbali mrefu  kufuata huduma na kuwajengea uwezo madaktari wenyeji.

Aidha, Dkt Mwita ameainisha magonjwa ambayo wanakutana nayo wakati wa kutoa huduma kuwa ni matatizo ya figo, shida katika mfumo wa hewa  na matatizo ya njia za kupitisha damu ambapo kuna kifaa maalumu cha kupima moyo  ambacho kinapatikana hospital ya halmashauri.

“kwa matatizo ya moyo kwa watoto tukiyaongelea yapo mengi kuna yale ya kuzaliwa na tundu la moyo, wengine wanazaliwa na moyo mkubwa lakini mtoto anaweza kuvamiwa na wadudu kwnye koo na kusababisha madhara kwenye moyo” aliongeza
Akitoa shukrani kwa niaba ya waliopata matibabu ya kibingwa mama wa mtoto aliyezaliwa njiti Bi. Shose Exaud Mosha amewashukuru madaktari kwa kumsaidia kumhudumia mtoto wake na kuwashauri kina mama wenye watoto  wawalete kupata huduma.

Awali, Dkt Charles amefafanua kuhusu gharama za matibabu amesema  huduma hizo zitatolewa kwa utaratibu wa kawaida kwa mwananchi wenye bima hali kadharika mwenye pesa taslimu.



Previous Post Next Post