Ticker

6/recent/ticker-posts

WANATAKIWA KUONGEZA UZALISHAJI WA MBEGU BORA ZA KILIMO ILI KUFIKIA MALENGO YA SERIKALI

Na Lucas Raphael,Dodama  

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA)   Leo Mavika amewataka Maafisa Kilimo wa Wakala wa Mbegu za kilimo kuhakikisha wanaongeza Uzalishaji wa Mbegu bora za kilimo ili kuweza kufikia Malengo yaliyowekwa na serikali.

 

Alitoa kauli hiyo  wakati akifungua Mafunzo ya Siku Tatu ya  Technolojia za Uzalishaji wa Mbegu bora za kilimo kwa maafisa kilimo wa ASA Mkoani Dodoma yanayotekelezwa kupitia programu ya kuendeleza kilimo na Uvuvi - AFDP.

 

Alisema kwamba wataalam waliohudhuria Mafunzo hayo wanapaswa kuzingatia Elimu itakayotolewa na wataalam ili kuleta ufanisi kwenye mashamba ya Taasisi.

 

Mavika alisema kwamba ASA inajukumu kubwa la kuhakikisha inazalisha Mbegu bora Kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya Nchi na kuepuka kuagiza Mbegu za kilimo kutoka Nje ya Nchi

 

Aliendelea na kusema “ Wakala wa Mbegu za kilimo ASA ina kipaumbele cha kuzalisha mbegu za Mazao 13 ambazo zinapaswa kupatikana wa wingi ikiwepo zao la Mahindi, Alizeti,Mpunga pamoja na Mazao mengine” Bw. Mavika


Aidha Mtendaji Mkuu huyo alisema Wakala wa Mbegu za kilimo ASA inatakiwa kuchangia kwa sehemu kubwa  uzalishaji wa Tani 127,650 ambazo ndio mahitaji halisi ya Nchi.

 

Alibainisha kwamba  Malengo ya Taasisi ni kuona mabadiliko makubwa baada ya Mafunzo hayo katika Mashamba kutokana na kupewa Mafunzo bora ya Uzalishaji wa Mbegu kwa Technolojia za kisasa kutoka kwa wataalamu waliobobea watakaowasilisha mada.

 

Mavika alipongeza Mafunzo hayo ya Programu ya kuendeleza kilimo na Uvuvi -AFDP yatasaidia kukuza uelewa kwa watumishi nakusaidia kufikia Malengo.

 

Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Emmanuel Maziku alisema Mradi huo unatekelezwa kwenye Mashamba matatu ambayo ni Shamba la Kilimi Nzega, Shamba la Msimba Kilosa Mkoani Morogoro. 

 

Alisema Mradi huo unatekeleza mambo mbalimbali kama vile karakana,majengo ya ofisi,Ukarabati wa Nyumba za watumishi,ujenzi wa Ghala la kuhifadhia Mbegu Kilimi pamoja na kununua Mtambo wa kuchakata Mbegu.

 

Aidha alisema baadhi ya Malengo ya Mradi huo nikuongeza Uzalishaji wa Mbegu pamoja na kuhamasisha sekta Binafsi kuzalisha Mbegu bora za kilimo.Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA)   Leo Mavika akizungumza na Maafisa Kilimo wa Wakala wa Mbegu za kilimo mkoani Dodoama .

 

Post a Comment

0 Comments