HUDUMA ZA KISHERIA KUSOGEZWA KARIBU NA WANANCHI











Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari ametembelea Jengo la Ofisi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali lililoko jijini Arusha tarehe 21 Novemba 2024.

Jengo liko katika hatua ya ujenzi na likikamilika litasaidia kusogeza huduma za Sheria kwa wananchi pamoja na vituo jumuishi ambapo jengo hilo litatoa huduma zote za kisheria kwa wananchi.

“lengo letu ni kukamilisha ujenzi wa jengo hili na kurahisisha upatikanaji wa huduma za Kisheria kwa Wananchi husasani wa Jiji la Arusha na maeneo ya jirani”. Alisema Mhe. Johari

Katika hatua nyingine Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema Jengo hilo mpaka kukamilika kwake litagharimu kiasi cha zaidi ya Shilingi Bilioni 3 ambapo litaweza kuhudumia mikoa miwili, Arusha na Manyara hali itakayopelekea kufanya huduma hizo kusogezwa kwa ukaribu zaidi.

Juhudi za utafutaji wa fedha kwa awamu ya mwisho ya kumalizia jengo hilo bado zinaendelea na baada ya kukamilika kwa jengo hilo wananchi watapata huduma za Kisheria kwa urahisi na haraka hivyo kusaidia utoaji wa haki kwa wananchi wa Jiji la Arusha, Mkoa wa Manyara na maeneo ya jirani.
Previous Post Next Post