JUMLA YA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA 570. WALA KIAPO CHA KUTUNZA SIRI PAMOJA NA KIAPO CHA UTII NA UADILIFU MANISPAA YA SHINYANGA.

MSIMAMIZI wa uchaguzi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius R.Kagunze amewaapisha jumla ya Wasimamizi wa vituo vya Kupigia kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 570. Kiapo cha Kutunza Siri pamoja na Kiapo cha Utii na Uadilifu.Uapicho huu Umefanyika leo Novemba 24, 2025 Katika Ukumbi wa Mikutano Shule ya Sekondari  Wasichana iliyopo kata ya Ndembezi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza baada ya kuwaapisha viapo hivyo Mwl.Kagunze  amewata Wasimamizi hao kuzingatia viapo hivyo kama walivyo apa.
"Jinsi mlivyoapa Leo kiapo Cha uamunifu na uadilifu ndivyo hivyo nendeni mkavitendee kazi viapo hivi, mmeteuliwa si kwa bahati mbaya Bali serikali inaimani kubwa sana na ninyi, endapo mtakiuka viapo hivi hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu yenu". amesema Mwl. Kagunze. Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Viapo hivyo vimeenda sambamba na kuwapatia mafunzo na kuwajengea uelewa Wasimamizi hao juu ya zoezi Zima la Uchaguzi ambapo Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Ndg  Charles Kafutila ameeleza namna ya utaratibu wa upigaji kura pamoja na kuwatambua wapiga kura waliojiandikisha kwenye daftari la Mkazi wa eneo husika pamoja na kutumia vitambulisho mbalimbali kama vile Kitambulisho Cha mpiga kura, na vitambulisho vingine vinavyotambulika. “wapiga kura wataruhusiwa kupiga wale tu waliojiandikisha kwenye daftari la mkazi wa eneo husika, haitaruhusiwa kwa mtu yeyote kupiga kura nje ya eneo lake la makazi au kwa ambaye hayupo kwenye orodha ya wakazi husika, lakini pia Mpiga kura hatoruhusiwa kuingia na simu ya mkononi kwenye chumba cha kupigia kura amesema” Ndg Kafutila.Katika hatua nyingine Ndg Kafutila amesema Vituo vitafunguliwa kuanzia saa mbili kamili asubuhi(2:00)  na kufungwa saa kumi kamili  jioni (10:00) hivyo haitaruhusiwa kwa Mtu yoyote kupiga kura nje au baada ya muda elekezi.Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika jumatano ya Novemba 27,2024 ambapo Manispaa ya Shinyanga ina kata 17, vijiji 17, vitongoji 84 na mitaa 55,Viogozi watakaochaguliwa kupitia uchaguzi huo wa Serikali za mitaa ni pamoja na Wenyeviti wa Mitaa, vijiji na vitongoji pamoja na wajumbe wao.


 

Previous Post Next Post