Chama cha mapinduzi CCM katika jimbo la Msalala wilayani Kahama,kimezindua rasmi kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu 2024 huku suala la kuilinda amani ya nchi likisisitizwa katika kipindi chote cha kampeni.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo mgeni rasmi ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga amewataka wapiga kura wa jimbo la Msalala kutokukubali kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani iliyopo huku akiwasihi kuwachagua viongozi wanaotokana na chama hicho kwani ndicho chama pekee kitakachowaletea maendeleo.
Awali mbunge wa jimbo la Msalala Iddi Kassim Iddi alieleza miradi iliyotekelezwa na serikali katika jimbo hilo, na kwamba kitendo cha wananchi kuendelea kukichagua chama hicho ni kuchagua maendeleo zaidi katika maeneo yao.
Naye mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi Taifa (wilaya ya Kahama) CDE Edwin Nyakanyenge akatoa pongezi zake kwa wanamsalala kwa kuitikia kwa wingi katika uzinduzi huo na kusisitiza kura zote kwa CCM.