Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga, Dkt. Elisha Robert, kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mwl. Alexius R. Kagunze, wanawatangazia wananchi wote kuwa kuanzia tarehe 4 hadi 10 Novemba 2024, kutakuwepo na huduma za matibabu ya kibingwa katika hospitali ya Manispaaya Shinyanga.
Huduma zitakazotolewa ni pamoja na:
Huduma za afya kwa watoto,
Huduma za afya ya uzazi, wajawazito na magonjwa ya wanawake,
Huduma kwa magonjwa ya ndani kama shinikizo la damu na kisukari,
Huduma za upasuaji,
Huduma za ganzi na usingizi,
Huduma za kinywa na meno,
Huduma za mifupa na majeraha.
Malipo kwa huduma hizi yatafanywa kwa njia ya Cash, NHIF, na ICHF.