MAKUNDI MAALUM YAASWA KUJITOKEZA KUSHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA


Mbunge Jimbo la Rorya Mhe.Jafari Wambura Chege amekutana na kuzungumza na wazee wilayani rorya ambapo lengo ni Kuwahasa wazee kujitokeza kushiriki uchaguzi na kuchagua Viongozi watakao waletea maendeleo ndani ya maeneo yao.

Akizungumza na wazee hao Mhe Chege amewataka wazee wajitokeze kwa wingi kushiriki uchaguzi, kwani uchaguzi huo ndo utakua na maamuzi ya kimaendeleo ndani ya miaka Mitano.

Aidha ameomba wazee  Wakawe hamasa na Washauri kwa wananchi wengine pindi wanapokua katika maeneo na familia zao.

"Wazee wangu leo tumekutana hapa kwa lengo kuu la kutiana hamasa na kukumbushana mengi yanayohusiana na uchaguzi unaokuja siku chache za mbele, Niwaombe Mjitokeze kwa wingi kwaajili ya kushiriki na kupiga kura ili kuchagua Viongozi watakao tuletea maendeleo ndani ya Vijiji na  vitongoji vyetu." Amesema Mbunge Chege.

Pia amewataka kuendelea kumsemea na  kumuombea Mhe Rais Samia Suluh Hassan kwa maendeleo mengi na  makubwa anayoendelea kuwaletea ndani ya Jimbo la Rorya.
 
Mhe Jafari amemaliza kwa kuwaahidi kuendelea kuwapa ushirikiano kila wakati kuhakikisha  wanaendelea kuijenga rorya mpya.

Previous Post Next Post