MAMENEJA RASILIMALIWATU KATIKA SEKTA YA UMMA AFRIKA WAMUUNGA MKONO RAIS DKT. SAMIA KUTANGAZA SEKTA YA UTALII WA TANZANIA

 

Rais wa Mtandao wa Mameneja wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akizungumza wakati Wajumbe wa Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Meneimenti ya Utumishi wa Umma na Utawaloa Bora wakifurahia kufika Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro baada ya kuhitimishwa Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Mjumbe wa Mtandao wa Mameneja wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) kutoka nchini Kenya akielezea namna alivyofurahia kuona wanyama na vivutio mbalimbali vilivyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro wakati wajumbe wa Mtandao wa Mameneja wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro mara baada ya kuhitimishwa Mkutano wa 9 wa APS-HRMnet uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Rais wa Mtandao wa Mameneja wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi (kushoto) akiteta jambo na Makamu wa Rais wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) Bw. James Wasagami walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro mara baada ya kuhitimishwa Mkutano wa 9 wa APS-HRMnet uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).


Na. Veronica Mwafisi-Arusha


Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) wamemuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutangaza sekta ya utalii katika nchi zao baada ya kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro ambayo ni moja ya vivutio maarufu duniani.

Akiongoza ziara ya Mameneja hao baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano Mkuu wa 9 wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet), Rais wa Mtandao huo ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi amesema waliona ni vema Mameneja hao kutoka nchi mbalimbali wakatembelea Hifadhi hiyo ili kuunga mkono jitihada za Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mstari wa mbele kutangaza sekta ya utalii ili kukuza uchumi wa Tanzania.

“Tuliona si jambo jema viongozi hawa wa Rasilimaliwatu wakarudi nchini kwao bila kufanya utalii, hivyo tukaamua kuratibu safari ya kwenda Ngorongoro kwani kwa kufanya hivyo tunaamini watatusaidia kwenda kutangaza utalii wa Tanzani katika nchini zao na kukuza pato la taifa.” Bw. Daudi amesisitiza.

Bw. Daudi amesema Mameneja hao wameweza kuona vivutio mbalimbali katika Hifadhi hiyo ya Ngorongoro ikiwemo wanyama, mandhari ya kuvutia pamoja na kujifunza masuala mbalimbali.

Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) uliofunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan umehitimishwa rasmi baada ya kufanyika kwa muda wa siku nne kuanzia tarehe 4 hadi 7 Novemba, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) jijini Arusha.

Mkutano huo ulibebwa na Kaulimbiu isemayo ‘Utawala Stahimilivu na Ubunifu: Kukuza Sekta ya Umma ijayo kupitia Uongozi wa Rasilimaliwatu’.
Previous Post Next Post