Picha ya Makabidhiano ya Vipaza sauti 17 Kutoka kwa Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mhe.Patrobas Katambi wa tatu kutoka kulia
Kuelekea katika uchaguzi wa
serikali za mitaa chama cha mapinduzi (CCM) kimeanza mikakati ya utekelezaji wa
kampeni zinazoanza kesho tarehe 20 November 2024 ambapo mbunge wa jimbo la
Shinyanga mjini Patrobas Katambi ametoa vipaza sauti 17 vyenye thamani ya shilingi milioni tisa
vitakavyorahisisha zoezi la kampeni kwa kata
zote kumi na saba za jimbo hilo
Akizungumza katika hafla fupi ya
kukabidhi spika hizo Katambi amewataka wanachama wa chama hicho kuhakikisha
wanatafuta kura ili kukipa ushindi chama hicho katika uchaguzi wa serikali za
mitaa lakini pia katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2025.
“Sisi Kama Chama tawala
tunatakiwa kuwa na umoja tushikamane na tupendane ili kushinda uchaguzi huu,
Mhe. Rais katuletea miradi mingi sana ya maendeleo katika kata zetu, maendeleo
hayo yanakuja kutokana na utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi, msingi
bora wa maendeleo ni kuchagua viongozi wa
serikali za mitaa wa (CCM) hivyo twendeni tukawahimize wananchi kuchagua
viongozi walioteuliwa na chama cha mapinduzi ili miradi inayoendelea katika
maeneo yetu iweze kukamilika”. Amesesema Katambi.
Katika hatua nyingine Mbunge Katambi
amesisitiza vifaa hivyo kutumika kwa usahihi ili ziweze kuwaingizia kupato
kitakachowasaidia kutatua changamoto mbali mbali za kiofisi.
“vifaa hivi tendeni kukavitunze
na kuvitumia kwa matumizi sahihi, kunamatukio mengi sana yanahitaji vipaza
sauti, kama sherehe ndogo ndogo kama kipaimara, Send Off tuweke uratibu mzuri lakini
Kama ikitikea janga lolote vitumike bure lakini kwa usimamizi sahihi tusiwatoze
pesa wananchi kwa majinga kama hayo. Tutambue kabisa imetolewa kwa chama ngazi
ya kata”. Ameongeza Katambi.
Awali akitoa hotuba ya utangulizi
katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Shinyanga mjini Hamisa Chacha amewaomba wanachama wa chama
hicho kumaliza tofauti na makundi
yaliyotokana na uchaguzi wa kura za maoni badala yake wake kitu kimoja kwa kuunga mkono wagombea waliopendekezwa na
chama cha mapinduzi.
Ndugu zangu Wana CCM viongozi hawa waliotruliwa na
viongozi wetu kugombea nafasi mbalimbali twendeni tukaunge kwa sababu viongozi wetu
wamewapima wakawaona wanafaa, tendeni tukawaombee kura za ndio kwa wananchi ili
chama chetu kiweze kupata ushindi katika maeneo yote. Amesema Hamisa