Na Mapuli Kitina Misalaba
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias
Ramadhan Masumbuko, amewataka Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA)
katika Wilaya ya Shinyanga kushughulikia haraka uboreshaji wa barabara
inayoelekea dampo la taka, ili kuondoa usumbufu unaojitokeza hasa wakati wa
mvua.
Akizungumza leo katika kikao cha Baraza la Madiwani,
Meya Masumbuko ametoa agizo hilo kufuatia hoja ya Diwani wa Kata ya Kizumbi, Mhe.
Reuben Kitinya, aliyetoa taarifa juu ya changamoto zinazokabili magari
yanayokusanya taka kutoka kata mbalimbali za manispaa hiyo kupeleka kwenye
dampo.
Kitinya ameeleza kuwa barabara hiyo siyo rafiki kwa
sasa, kwani ina mabonde mengi yanayosababisha usumbufu mkubwa kwa magari
yanayosafirisha taka.
“Nakumbuka
hata Mwaka jana hali ya mvua ilisababisha ile barabara kuwa mbaya sana kuna
marekebisho yalifanyika lakini si kwa kiwango ambacho kilitarajiwa sasa masika
iko karibu kuna mpango gani sasa wa kuimarisha ile barabara ili isiwepo tena
changamoto ya kutokufikishwa takataka kwenye eneo husika”.amesema
Kitinya
Meya Masumbuko amesisitiza kuwa TARURA inapaswa
kuchukua hatua za haraka na ametoa muda wa wiki moja kwa wakala huo kutoa
mrejesho wa hatua za awali za kuboresha barabara hiyo.
“Ni kweli kulikuwa na changamoto ya hiyo barabara
siyo tu Mwaka jana hii ni awamu ya tatu na tumkuwa tukipokea taarifa mbalimbali
kutoka ofisi ya TARURA lakini hatujaona hatua zimechukuliwa sasa naomba ulichukue
kama ni jambo la muhimu na ni jambo la
msingi na liwe la muda mfupi”.
“Halmashauri
yetu imekuwa ikijitahidi sana kuhakikisha kuwa hali nzuri ya usafi kwa maana ya
kulinda mazingira yetu na afya za jamii wanaoishi ndani ya Halmashauri hii sasa
kama tutashindwa kuzifikisha taka mahara panapohusika maana yake maana yake
tutarajie matokeo haribifu katika maeneo mbalimbali na sisi hatutakubaliana na
jambo hili naomba ulichukulie umuhimu na utupe taarifa ndani ya wiki moja kwenye
ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri”.amesema Meya Masumbuko
Kwa upande wake, Mhandisi Kulwa Maige, ambaye
amezungumza kwa niaba ya Meneja wa TARURA Wilaya ya Shinyanga, amethibitisha
kupokea maelekezo hayo na ameahidi kushughulikia changamoto hiyo.
Barabara ya kuelekea kwenye dampo la taka kutoka mjini Shinyanga ni yenye urefu wa kilomita 4.2.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias
Ramadhan Masumbuko, akiwasisitiza Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini
(TARURA) katika Wilaya ya Shinyanga kushughulikia haraka uboreshaji wa barabara.
Akizungumza kwa niaba ya Meneja wa TARURA Wilaya ya
Shinyanga Mhandisi Kulwa Maige, amethibitisha kupokea maelekezo hayo.
Diwani wa Kata ya Kizumbi Mhe. Reuben Kitinya, awali akiuliza maswali.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban akizungumza kwenye baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Novemba 1, 2024.Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze akizungumza kwenye baraza hilo.Mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ukiendelea leo Novemba 1, 2024 ambapo pamoja na mambo mengine madiwani wamepokea na kujadili taarifa mbalimbali za Halmashauri hiyo.Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Mhe. Anord Makombe akitoa salamu zake kwenye baraza la madiwani leo Novemba 1, 2024.Mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ukiendelea leo Novemba 1, 2024 ambapo pamoja na mambo mengine madiwani wamepokea na kujadili taarifa mbalimbali za Halmashauri hiyo.Mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ukiendelea leo Novemba 1, 2024 ambapo pamoja na mambo mengine madiwani wamepokea na kujadili taarifa mbalimbali za Halmashauri hiyo.Mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ukiendelea leo Novemba 1, 2024 ambapo pamoja na mambo mengine madiwani wamepokea na kujadili taarifa mbalimbali za Halmashauri hiyo.Mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ukiendelea leo Novemba 1, 2024 ambapo pamoja na mambo mengine madiwani wamepokea na kujadili taarifa mbalimbali za Halmashauri hiyo.