Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini Ndg. Anord Makombe akishiriki kupiga kura uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika kituo cha kupigia kura Zahanati ya Bushushu kata ya Lubaga Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga
Mjini Ndg. Anord Makombe leo Novemba 27, 2024 ameshiriki kupiga kura Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa 2024 kwenye kituo cha kupigia kura Zahanati ya Bushushu
Kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni kutimiza haki yake ya Kikatiba.
Makombe Amesema ameshiriki kupiga kura ili kuchagua viongozi
hao wa serikali za mitaa, kwa sababu mfumo wa serikali unaanzia ngazi ya
chini,hivyo upatikanaji wa viongozi makini ngazi ya vijiji,vitongoji na mitaa,
ndiyo msingi imara wa utawala.
"Zoezi hili la uchaguzi linakwenda vizuri na wananchi wamejitokeza kupiga kura tena kwa amani na utulivu, na wasimamizi wa uchaguzi wanatoa maelekezo mazuri namna ya kupiga kura," amesema Ndg Makombe.