MSALALA YATENGA ZAIDI YA MILIONI 78 KWAAJILI YA LISHE


Halmashauri ya Wilaya ya Msalala imetenga bajeti ya zaidi ya shilingi milioni 78 kwa ajili ya kuchangia shughuli mbalimbali za lishe, huku wakina mama wakitakiwa kuzingatia makundi 6 ya vyakula ili watoto waweze kupata afya bora.


Kauli hiyo imetolewa leo Novemba 01, 2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya  Msalala Bi Rose Manumba wakati akizungumza na wakinamama wa Kata ya Segese katika maadhimisho ya siku ya Lishe duniani, ambapo amesema kushiba pekee sio lishe bora bali wanatakiwa kuzingatia namna sahihi ya uandaaji wa chakula kwa kuzingatia makundi yote ya vyakula.

“Wakina mama hakikisheni mnazingatia lishe bora kwa watoto wenu kwa kuzingatia makundi sita ya lishe ili kuondokana na magonjwa na hali ya udumavu’’ alisema Rose Manumba.

Katika hatua nyingine, Manumba amewataka wananchi waliojiandisha katika daftari la kudumu la mpiga kura na daftari la makazi washiriki katika zoezi la kupiga kura ifikapo novemba 27 mwaka huu 2024.

Nae, afisa lishe wa Halmashauri ya Msalala Peter Nganzo  ametoa mafunzo juu ya uandaaji wa chakula bora kilicho zingatia makundi yote ya chakula ili watoto waweze kuwa na lishe bora itakayo wasaidia katika makuzi yao na kutokupata magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora.

Katika maadhimisho hayo ya lishe yamehudhuriwa na wataalumu mbalimbali kutoka katika Halmashauri hiyo pamoja na wananchi wa Kata ya Segese.

Imetolewa na  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini






















Previous Post Next Post