Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga kimewataka wagombea Wote wa serikari za mitaa kufanya kampeni za kistaarabu ili kuwezesha mikutano hiyo kufanyika katika mazingira ya amani na utulivu hivyo kutoa nafasi kwa wananchi kusikiliza sera za wagombea.
Rai hiyo imetolewa leo na katibu wa siasa na uenezi wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Bwana Said Bwanga wakati akiwanandi wagombea wa chama hicho kwenye mkutano wa kampeini katika mtaa wa viwandani kata ya mjini .
Bwana Said Bwanga amewasisitiza wagombea wa chama hicho kutumia majukwaa ya kampeini kunadi sera zao , kwa lugha za kistaarabu badala ya kutumia lugha zinazochochea chuki na kuwagawa wananchi.
Kwa upande wake ngombea wa nafasi ya uenyekiti wa mtaa wa viwandani Ashiraf u Majariwa ambaye anaomba nafasi hiyo kwa mara ya pili amewaomba wakazi wa mtaa huo kuendelea kumwamini ili aweze kushirikiana nao katika hatua za kutatua kero na changamoto zilizopo.
Wagombea wa nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikari za mitaa wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga wanaendelea kunadi sera zao kwenye mikutano ya kampeini zilizoanza jana nchini kote.