RAIS SAMIA AAGIZA HATUA ZA HARAKA UOKOAJI MAJERUHI WA AJALI YA JENGO KARIAKOO DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa maagizo ya haraka kwa mamlaka mbalimbali kushirikiana kuhakikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi wa ajali ya kuanguka kwa jengo la ghorofa tano linafanikiwa.

Ajali hiyo imetokea leo asubuhi katika eneo la Kariakoo, jijini Dar es Salaam, ambapo taarifa za awali zinaonyesha idadi kadhaa ya watu wamejeruhiwa na wengine wakiwa bado wamekwama chini ya kifusi.

Katika maagizo yake, Rais Samia ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili, kushirikiana kwa karibu na Idara ya Menejimenti ya Maafa kuhakikisha kila hatua muhimu ya uokoaji inatekelezwa mara moja.

Zoezi la uokoaji linaendelea huku wananchi wakihimizwa kushirikiana na mamlaka kuhakikisha usalama katika eneo la tukio. Idadi kamili ya majeruhi na wahanga bado haijathibitishwa rasmi.

Misalaba Media tutaendelea kufuatilia maendeleo ya tukio hili na kuwapa taarifa zaidi kadri zinavyopatikana.

Previous Post Next Post