SAGINI AFANIKISHA MIL. 19 HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA JIPYA LA WAADVENTISTA WASABATO MIEMBENI BUNDA

Na Gabon Mariba, Mara.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria (Mb) Mhe. Jumanne Sagini amefanikisha kiasi cha shilingi 19,769,500/- katika Harambee ya Ujenzi wa Kanisa jipya la Waadventista Wasabato Miembeni katika Kata ya Bunda Stoo Wilaya ya Bunda Jimbo la Mara.

Katika Harambee hiyo Mhe. Jumanne Sagini aliambatana na Mbunge wa Jimbo Bunda Mjini Mhe. Jumanne Maboto, Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Mara Mhe. Ghati Chomete, Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa Ndg. Fidelis Kisuka, Mwenyekiti CCM Kata ya Kukirango Ndg. Mazera Kabazi, Mwenyekiti CCM Kata ya Sirorisimba Ndg. Ntang'ana Maroba, Diwani Kata V.M Wilaya ya Butiama Mhe. Amina Solis na Amos Marwa Mwenezi CCM Kata ya Sirorisimba.

Pia Mhe Sagini amewataka waumini wa kanisa hilo kuendelea kuliombea Taifa lao kwa ajili ya amani, upendo, na usalama na kujitikeza kwa wingi kwenye uchaguzi wa Serikali ya Mitaa unaotarajia kufanyika Tarehe 27 Novemba, 2024.

Kwa upande wake Mchungaji Winnah Malagila ambaye alimwakilisha Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Jimbo la Mara amewashukuru viongozi wa siasa, kidini na serikali walioshiriki harambee hiyo na kumuahidi Mgeni Rasmi Mhe. Jumanne Sagini kuwa viongozi watakuwa dini watakuwa sehemu ya juhudi zinazoendelea za kuhamasisha wananchi kushiriki katika kuimarisha amani na utulivu nchini kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Previous Post Next Post