SHINYANGA: UFUNGUZI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KUFANYIKA WILAYANI KISHAPU

 
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga kimepanga kufungua rasmi kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa katika Wilaya ya Kishapu, Kata ya Bubiki. Hafla hiyo itaanza saa 11 alfajiri na inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na wananchi wa eneo hilo.

Mgeni rasmi katika tukio hili atakuwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Mohamed Bashe, ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (MNEC). Pamoja naye, viongozi wengine wa chama watakaokuwepo ni pamoja na MNEC Gaspar Kileo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, Katibu wa CCM Mkoa Odilia Batimayo, na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa Richard Raphael Masele.

Hafla hii inalenga kuhimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kaulimbiu  ya mwaka huu, "Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi." Viongozi wataeleza mikakati ya chama ya kuhakikisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanafikiwa kupitia serikali za mitaa.

Endelea kufuatilia MISALABA MEDIA ili kupata habari mbalimbali 










Previous Post Next Post