TAASISI YA DESK& CHAIR FOUNDATION YAWAKUMBUKA WAFUNGWA MWANZA .

NA NEEMA KANDORO, MWANZA

TAASISI ya Desk &Chair ya Jijini Mwanza imekabidhi kisima kirefu cha maji walichochimba na kuwekea miundo mbinu ya kusambaza maji yenye thamani ya zaidi ya milioni 40 katika gereza la Butimba.

Akikabidhi kisima hicho jana Tarehe 14 /11/ 2024 Mwenyekiti wa taasisi hiyo Sibstain Meghjee alisema wametekeleza ahadi hiyo waliyotoa kwa asilimia 100 ambayo inauwezo wa kusambaza maji ikiwa na tenki la lita 10000 iliyounganishwa umeme wa njia tatu ili kuendesha pampu.

Kima hicho kitasaidia nyakati za ukosefu huduma hiyo kutoka Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mkoani Mwanza (MWAUWASA) ambapo itahudumia watu 3000 kwa siku.

Alisema vilevile wameweka tanki zingine tano za ujazo wa lita 1000 kila moja katika maeneo tofauti kwenye gereza hilo huku wakiwa wamejenga vilevile tanki lenye uwezo wa kutunza maji lita 15,000

Aidha pamoja na msaada huo vilevile wamekabidhi mbao tano za kufundishia elimu ya watu wazima,katoni tano za karatasi,madaftari 200,ndoo 10, kalamu na penseli, majora manne ya nguo, jagi za maji 120 na vitu vingine.

Meghjee alisema msaada huo umepatikana kupitia ufadhiri wa taasisi ya Kinship ya nchini Canada ambayo baada ya kuombwa msaada huo na gereza hilo waliwasiliana nao ili wasaidie kutoa huduma hiyo.

Vilevile taasisi hiyo ililipa kiasi cha sh 550,000 za luku kusaidia huduma ya nishati ya umeme kwenye gereza hilo kubwa mkoani Mwanza.

Ofisa Magareza mkoani Mwanza Masudi Kimolo alishukuru kupatikana kwa msaada huo na kusema hatua hiyo itawaondolea adha ya ukosefu wa maji iliykuwa inajitokeza kipindi yali[pokuwa yakikatika kwenye mabomba

Alisema msaada huo utasaidia watu waliopo kwenye gereza hilo katika kufanya usafi na kuendeshea shughuli za kilimo cha bustani katika eneo hilo.

Adha Mkuu huyo wa Magereza Mkoani Mwanza alisema msaada wa kisima hicho kirefu italeta faraja kubwa kwa gereza hilo la Butimba kwani adha ya maji imefanya wawe na malimbikizo ya deni la sh milioni 400.

Kimolo alisema serikali siku zote inaunga mkono jitihada zinazofanywa na wadau wa maendeleo hapa nchini katika kuunga mkono jitihada zake katika taifa letu




Previous Post Next Post