UJINGA NI JANGA KUBWA

UJINGA NI JANGA KUBWA

1. Ujinga hauui ila unatesa sana. Ukiwa mjinga utaliwa na kila mjanja. Inaitwa wajinga ndiyo waliwao. Ujinga ni mtaji wa matapeli ya kiroho na kimwili! 

2. Tapeli la kiroho linahitaji wajinga wengi liwauzie wokovu na wakati wokuvu anatoa Mungu! Tena bure bureeee!

3. Tapeli la kisiasa linahitaji wajinga wengi wa kulipigia kura hata kama halitekelezi ahadi zake. Mtalifanyaje na wakati linajua nyie ni wajinga tu? *Mwisho wa mwaka linakuja kuchukua kero zenu na si kutatua kero zenu!*

4. Tapeli la kielimu linahitaji wajinga wengi ili liwauzie elimu inayofuta ujinga bila kuongeza maarifa. Matokeo yake? *Jamii imejaa wasomi watafuta ajira na si watengeneza ajira. Hili ni janga!*

5. Tapeli la uganga wa kienyeji linahitaji wajinga wengi wa kuwapiga pesa bila kukamatwa na vyombo vya dola kwa sababu linajua wanaokwenda kwake ni wajinga. Litakupa masharti yasiyotekelezeka na utatoa hela maana linajua huja akili ya kujua kama linakudanganya.

7. Tapeli la serikali nalo linahitaji wajinga wengi la kuwauzia haki zao kwa kutoa kitu kidogo na wakati mtaani tunaambiwa nilitumishi la umma.

8. Tapeli la mapenzi litahitaji wanaume wengi wajinga wa kulilipia kodi, ada za watoto, saluni na outing zake zote! *Ukikutana nalo linakwambia yaani bebi uko peke yako na wakati linao tisa!*  Linajua huna akili ya kubaini uongo.

6. Tapeli la kizungu linahitaji wajinga wengi wa kuwapa misaada ili kuwafumba akili liendelee kuchuma mali za wajinga na wakati imeandikwa hakuna aliyeendelea kwa misaada!

7. Serikali ya kitapeli inahitaji wajinga wengi ili iendelee kufanya mambo yake bila bughudha yoyote. Wajinga wanaogopa sana serikali. Wajinga wakiona unahoji na kukosoa serikali wanakuonea huruma kwamba watakuu. Serikali haiui watu bhana!
 
9. Tapeli la mitandaoni linahitaji wajinga wengi ili liendelee kula na kuendesha maisha kwa jasho la wajinga. Wajinga ndo wanaopigwa pesa mitandaoni kila siku. Unapigiwa simu ati kuna fursa toa pesa na kweli unatoa. Wewe ni mjinga. Sikiliza *UKIONA JAMBO NI RAHISI KULIPATA HUO NI MTEGO, SHITUKA!*

10. Tapeli la kibiashara linahitaji wajinga wengi wa kuwapiga. Ukiwa mjinga sana utauziwa TECNO yenye cover la Iphone ukidhani ni Iphone maana wanajua mjinga hajui bei halisi ya Iphone og!

11. Ujinga unabeba umaskini! Ujinga unabeba maradhi; ujinga unabeba ujinga alisema Mzee Bagonza wa Kayanga Karagwe!

12. Ujinga unafanya watu wasiwe watu wa maana. Wanakuwa watu wa hovyo. Hawana thamani!

13. Ujinga ni kuwa uchi akilini. Ujinga ni mtu bila akili. Mtu bila akili ni mkurupukaji! Hana mipango! Yeye ana matukio! Tena ya ghafla kama chafya! 

14. Ujinga ni kufanya jambo lilelile kwa kutumia njia zile zile ukitegemea matokeo tofauti. 

15. Ujinga ni kulazimisha kufanana na wenzako na wakati Mungu kakuumba tofauti. Matokeo yake? Jamii yetu imejaa watu feki, ndoa feki, urafiki feki, imejaa maigizo. Sikiliza! *Ukiiga kunya kwa tembo utachanika*.

16. Ujinga ni kuutesa moyo kwa kusubiri vya kupewa na wakati maisha ni kutafuta cha bure ni kaburi. Hili nalo wajinga hawalijui.

17. Hata kuitikia kazi iendelee na wakati huna kazi, umekaa tu, unasubiri kulishwa na wakati umesoma ni sehemu ya ujinga. Tafuta kazi, ndiyo uwe na mamlaka ya kuitikia KAZI IENDELEE!

18. Ujinga ni janga linalotugharimu kama taifa. Tunahitaji nguvu kidogo tu kuendelea kuwa !

Previous Post Next Post