WATUMISHI WA TFS WAKUTANA JIJINI ARUSHA KUKUZA VIPAJI

 


Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania TFS imeandaa bonanza la michezo kwa lengo la kuwakutanisha watumishi mbalimbali kutoka katika kanda zote nane nchini kwa lengo la kutoa fursa kwa maafisa uhifadhi kukutana na kubadilishana mawazo

Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS Prof. Dos Santos Silayo akizungumza jijini Arusha na waandishi wa habari katika nusu fainali ya bonanza hilo amesema michezo hiyo ni sehemu ya kujenga afya ya akili na mwili Pamoja na kuondoa msongo wa mawazo.

Amesema hatua hiyo imetokana na uongozi wa  taasisi hiyo kufanya kazi katika mazingira magumu kutokana na majukumu yao ya kazi hivyo kupitia michezo kutawajengea uwezo wa kujiamini na uzalendo sambamba na kuweza kufanya kazi kwa pamoja na kuweka ari katika kazi ili kuweza kuwafanya wawe na nidhamu katika kazi.

"Katika kufanya hivi tunalenga kuwakutanisha watumishi wetu kutoka ngazi za chini kabisa na kuweza kufikia kwenye ngazi ya makundi ambapo malengo ni kuongeza idadi ya michezo kwa siku zijazo na idadi ya washiriki kwa kutumia uzoezi ambao tumeupata hapa."Alisema Prof. Silayo

Ameongeza kuwa wamekutana kwaajili ya michezo mikuu mitatu ambayo ni Soka,mpira wa Pete pamoja mchezo wa riadha ambapo matarajio yao ni kuongeza michezo mingine zaidi kusudi timu ziweze kuwa nyingi zaidi na kukaa kambia kwa muda mrefu na kupata timu iliyo bora zaidi.

Ameeleza kuwa kwa kufanya hivyo wanategemea TFS itakuwa kinara wa kuonyesha njia katika taasisi za uhifadhi ambazo zinaweza kuletwa pamoja kujenga umoja katika utendaji kazi na kuibua vipaji mbalimbali ikiwemo vya uongozi, kimichezo na kinidhamu katika utendaji wao ambao utawasaidia kuwakuza na kuwalea katika taasisi ili kuweza kulinda rasilimali nyuki,misitu na kuwa wazalendo wa taifa lao wenyewe.

Naye Mjumbe wa Bodi TFS Bi. Fiencia Mustapha Kiure amesema uwepo wa wafanyakazi wa TFS ni faraja kwao na wamefurahishwa na michezo wanayoifanya kwani inawapa faida kubwa ambapo wanayofamefurahishwa kuona jambo hilo linafanyika kwa kukutanisha wafanyakazi kutoka sehemu mbalimbali za nchi kwaajili ya kucheza na kufurahi kwa pamoja.

Amesema kuwa mbali na utunzaji wa misitu wanazingatia masuala ya afya kutokana na michezo kuwa sehemu ya afya ya mwili ambapo kupitia michezo hiyo imeweza kuwaleta pamoja wahifadhi kutoka nyanda mbalimbali ili kuweza kujifunza zaidi masuala ya misitu na namna ambavyo wengine wamefanikiwa katika uboreshaji wa misitu na kwenda kutekeleza kwa nafasi zao.

"Sisi tumejumuika ili tuweze kuona timu mbalimbali na hapa nusu fainali kati ya kanda ya kaskazini na kanda ya ziwa zinaendelea kucheza na tunategemea kupata mshindi hapo kesho kwenye fainali kwa upande wa mpira wa miguu na kwa upande wa mpira wa pete vivyo hivyo."alisisitiza Bi.Fiencia Mjumbe wa Bodi TFS

Sambamba na hayo Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya TFS nchini Enock Emmanuel Nyanda akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo amesema lengo kuu la mashindano hayo ni kuimarisha ushirikiano, urafiki pamoja na afya ambapo amesema upo umuhimu kwa wafanyakazi kukaa pamoja, kushirikiana na kufanya kazi kwa urafiki.



Previous Post Next Post