WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Novemba 22, 2024 anamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa kongamano la tano ya Maendeleo ya Biashara na Uchumi linalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina jijini Dodoma.
Kongamano hilo linatoa fursa kwa wanafunzi, taasisi za elimu, wataalamu wa sera, wajasiriamali, na wadau kutoka sekta ya umma na binafsi kujadili na kushauri kuhusu masuala yanayohusiana na mazingira ya biashara na uwekezaji.
Pia, Kongamano hilo linatoa fursa ya kutafuta suluhisho la changamoto za taaluma ya biashara na uchumi na kuongeza ufanisi katika mifumo ya biashara na uwekezaji ili kuongeza kasi ya maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii.