ZPDB YATAKIWA KUZINGATIA MIUNDOMBINU TSFIKI KWA WATU WENYE ULEMAVU











Na Rahma Khamis Maelezo.

Makamo Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Baraza la Wawakilishi ameitaka Taasisi ya Afisi ya Rais, Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini Zanzibar (ZPDB) kuzingatia masuala ya Watu wenye ulemavu ili kuongeza kasi ya ujumuishi.

Wajumbe wa Kamati hiyo chini ya Makamo Mwenyekiti wake Mhe. Mussa Foum Mussa wameyasema hayo huko Madema mara baada ya kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa mpango kazi kwa kipindi cha Robo ya kwanza (Julai-September) 2024-2025.

Amesema baadhi ya Miundombinu inayojengwa ikiwemo Majengo hayakuzingatia masuala ya Watu wenye Ulemavu jambo ambalo linakosa ujumuishi wa Watu hao.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu Mhe. Ali Suleiman Ameir (Mrembo) amesema suala la Miundombinu limepewa kipaombele hivyo watahakikisha wanafanya kila jitihada ili kila mmoja afikie malengo yaliokusudiwa.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango kazi kwa kipindi Cha robo ya kwanza (Julai_September) 2024-2025 Afisa Mtendaji Mkuu, Taasisi ya Afisi ya Rais Ufatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (ZPDB) Prf. Muhammed Hafidh Khalfan amesema Taasisi hiyo ilipangiwa TZS ,577.2 Milioni Kati ya fedha hizo TZS,253.8 Milioni kwa ajili ya matumizi ya menineyo na TZS,323.3 Milioni kwa ajili ya Mshara ambapo hadi kufikia September, 2024, imeingiziwa jumla ya TZS 384.2 Milioni sawa na asilimia 66.6.
Previous Post Next Post