ASKOFU SANGU KUADHIMISHA MISA YA MKESHA WA MWAKA MPYA KATIKA KANISA KUU LA MAMA MWENYE HURUMA NGOKOLO MJINI SHINYANGA

 Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, leoJumanne tarehe 31.12.2024, ataadhimisha Misa ya mkesha wa mwaka mpya, katika Kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga.

Misa hiyo itaanza saa 4:00 usiku, ambapo pamoja na mambo mengine, imelenga kuwapa fursa ya pekee waamini kumshukuru mwenyezi Mungu kwa Baraka ambazo amewajalia katika kipindi cha mwaka unaomalizika wa 2024, na kuomba Baraka kwa mwaka ujao wa 2025.
Kesho Jumatano tarehe 01.01.2025, Askofu Sangu ataongoza Misa ya shukrani ya Mwaka mpya 2025 katika Kanisa kuu Ngokolo, ambayo itakwenda sanjari na kufunga nadhiri za kwanza na kurudia nadhiri kwa watawa wapatao 29, wa Shirika la kijimbo la Maria Mtakatifu Mama wa huruma.
Kati ya hao, wanane miongoni mwao watafunga nadhiri za kwanza, ambapo 15 watarudia nadhiri kwa mara ya kwanza, na wengine 6 watarudia nadhiri kwa mara ya pili.
Misa ya mwaka mpya inatarajiwa kuanza saa 3:30 asubuhi.
Misa zote zitarushwa Redio Faraja na kupitia ukurasa wa Facebook
Previous Post Next Post