BARRICK NA TAIFA GAS WAENDELEA KUELIMISHA UMMA DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KATIKA ENEO LA NORTH MARA


Na Mwandishi wetu, Misalaba Media 

Elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kati ya wadau wanaoshirikiana kati ya Barrick na Taifa Gas yawafikia wananchi wanaozunguka Mgodi wa North Mara.

Kampuni ya Barrick Nchini Kupitia Mgodi wake wa North Mara kwa Kushirikiana na Kampuni ya Taifa Gas Wameendelea kutoa Elimu juu ya kupinga Ukatili wa Kijinsia Wilayani Musoma Mkoani Mara kwa Wananchi wanaozunguka Mgodi wa North Mara.

Aidha Elimu hiyo Iliambatana na Kampuni ya Taifa Gas Kugawa Majiko ya Gas ya Kupikia kwa kaya zaidi ya 222 zinazozunguka Mgodi huo.

Licha ya Kupatiwa Elimu juu ya kupinga Ukatili wa kijinsia Washirika walipatiwa mafunzo ya matumizi ya nishati salama kutoka kwa mkufunzi wa nishati kutoka Taifa Gas ambayo ni mdau katika kampeni hii, Praygod Ole Naiko ambaye alisema kuwa kampuni hiyo iko mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhimiza jamii kutumia nishati safi ya kupikia kwa lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira.



























Previous Post Next Post