Na Mapuli Kitina Misalaba
Hatua ya robo fainali ya Ligi ya Makamba Lameck
(Krismas Cup) imeendelea leo Disemba 8, 2024 katika uwanja wa Mhangu, kata ya Salawe, ambapo
Beya FC imeibuka mshindi kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Ikonongo FC maarufu
kama Mahakama na kwamba goli hilo pekee limefungwa na nyota wa mchezo huo Bwana
Mussa Lukaku.
Akizungumza kwa niaba ya msimamizi wa ligi hiyo,
Placid Thomas amesema kesho Jumatatu ligi hiyo haitaendelea kutokana na
maadhimisho ya Siku ya Uhuru yatakayofanyika katika uwanja huo kimkoa.
Hata hivyo, ligi itaendelea tena Jumanne kwa mechi
nyingine ya robo fainali kati ya Mahando FC na Mwasenge FC, huku Salawe FC na
Mwabenda FC wakitarajiwa kuchuana Jumatano ili kukamilisha hatua ya robo
fainali na kuingia nusu fainali.
Wachezaji, makocha, na mashabiki wa ligi hiyo wameendelea
kumpongeza mdhamini wa mashindano hayo, Makamba Lameck, kwa juhudi zake za
kukuza michezo na kuimarisha afya kupitia ligi hiyo.
Ligi ya Krismas Cup, inayodhaminiwa na Makamba Mussa
Lameck kupitia kampuni yake ya MCL inayojihusisha na biashara ya nafaka,
inalenga kukuza vipaji vya michezo na kuchochea maendeleo ya kimichezo mkoani
Shinyanga.
Mashindano hayo yanatarajiwa kufikia kilele tarehe
17 Desemba 2024 ambapo mshindi wa kwanza hadi wa tatu watapata zawadi.
Endelea kufuatilia MISALABA MEDIA kwa taarifa za michezo na matukio yote ya Ligi ya Makamba Lameck.
Placid Thomas, akizungumza kwa niaba ya msimamizi wa
ligi ya Krismas CUP.
Placid Thomas, akizungumza kwa niaba ya msimamizi wa ligi ya Krismas CUP.