CHADEMA SHINYANGA WATOA TAMKO LA KUUNGA MKONO MAAZIMIO YA KAMATI KUU YA CHAMA


CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).
         MKOA WA SHINYANGA
S.L.P.170,
Shinyanga, Tanzania.
Desemba 11, 2024

          TAARIFA KWA UMMA

TAMKO LA KUUNGA MKONO MAAZIMIO YA KAMATI KUU YA CHAMA

Baraza la Uongozi Mkoa wa Shinyanga lilipokea maazimio ya Kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 02 Desemba, 2024 na maazimio hayo yalisomwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Freeman Mbowe jana tarehe 10 Desemba, 2024.

Pamoja na maazimio mengine. Tunaelekeza ngazi za Wilaya, Majimbo, Kata, Matawi na Misingi kuanza kutekeleza mapema mambo yafuatayo;

Mosi, kuanza mara moja kuwahimiza wananchi kuwanyima ushirikiano wowote viongozi wote wa vitongoji, serikali za vijiji na mitaa pamoja na watendaji wa mitaa/Vijiji na kata walioshiriki kuharamisha uchaguzi wa tarehe 27 Novemba 2024.

Pili, Kwamba, viongozi wa wilaya na majimbo, wawasiliane na wadau wote waliopo kwenye majimbo na wilaya zao wakiwemo vyama vya siasa, taasisi za dini, makundi ya kijamii, asasi za kiraia, wasomi, wakulima, wafanyabiashara, watu mashuhuri katika jamii na wananchi wote kuunganisha nguvu za pamoja ili kuwaeleza namna Uchaguzi  ulivyokuwa si huru, haki na kutafuta namna ya  kudai mifumo huru ya uchaguzi nchini.

Tatu, kuendeleza vuguvugu la kudai Katiba mpya na kufanya maboresho ya Sheria na mifumo ya Uchaguzi. Na kuendelea kushinikiza kupatikana Tume huru ya Uchaguzi.

Nne na mwisho, tunatoa wito wa kuimarishwa kwa mfumo wa CHADEMA Familiy katika ngazi za chini ili kusaidiana kwa wana CHADEMA na wanajamii wanaotuunga mkono katika masuala ya kijamii katika maeneo yetu.

Aidha, CHADEMA Mkoa wa Shinyanga inalaani ukamatwaji wa viongozi na wanachama kabla, wakati na baada ya uchaguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi na kuwa kilichotokea tarehe 27 Novemba, 2024 hakikuwa uchaguzi halali, huru na haki bali uporaji na uhalifu wa kiuchaguzi.



No Hate, No Fear!

Emmanuel Ntobi
Mwenyekiti wa CHADEMA
Mkoa wa Shinyanga.
Desemba 11, 2024.
Previous Post Next Post