HATI YA ARDHI HAIAZIMISHI: PINDA


Katavi 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amekabidhi jumla ya hati miliki za kimila 350 kwa wananchi wa kijiji cha Ikulwe kilichopo Kata ya Majimoto katika halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi.


Tukio hilo la ugawaji wa hatimiliki za kimila limefanyika Jumapili 01 Desemba 2024 katika mkutano wa kijiji uliohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Majid Mwanga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Mpimbwe Bi. Shamim Mwariko.

Mhe pinda amewataka kuhakikisha hati miliki hizo hawazitoi kwa mtu yeyote kwani ni nyaraka za siri ambayo itamwezesha mwananchi kama dhamana ya kuaminiwa kupata mikopo kupitia taasisi za kifedha 

Mhe. Pinda amewataka wananchi wa Ikulwe kutunza hatimiliki hizo sehemu salama ili zisiharibike mathalani na maji. 

Sambamba na hilo Naibu Waziri Mhe. Geophrey Pinda amewahakikishia wananchi kuwa hati hizo zitaenda kupunguza migogoro ya ardhi baina yao kwa kuwa zoezi la utambuzi wa maeneo na uwekaji alama za msingi limefanyika na wananchi kupatiwa hati.







Previous Post Next Post