LEO NDIO LEO! CHALINZE FESTIVAL FUNGA MWAKA BONANZA NDANI YA CHALINZE, KIKWETE AGAWA VIFAA

CHALINZE KUPENDEZA MWAKA MPYA.

_Rais Mstaafu wa Awamu ya 4 Dkt. Jakaya Kikwete ataongoza Bonanza kama Mgeni rasmi, Bongo Muvi ndani_ 

Mbunge wa Chalinze na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira, na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete anafunga mwaka na Bonanza kubwa la kufunga mwaka la Chalinze Festival Leo Jumanne Disemba 31, 2024 kwenye Uwanja wa Polisi Chalinze kuanzia majira ya saa 9 alasiri. Tayali Waziri Kikwete amegawa vifaa kwa ajili ya Bonanza hili.

Patapigwa michezo miwili mikali kati ya Chalinze United Vs Mdaula United na ule wa Watumishi CDC HQ Vs Wasanii Bongo Movie. Mgeni rasmi kwenye Bonanza hili la aina yake atakuwa ni Rais Mstaafu wa Awamu ya 4 Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Usipange kukosa.





Previous Post Next Post