Na Mapuli Kitina Misalaba
Ligi ya Makamba Lameck (Krismas Cup 2024) inaendelea
kwa kasi kwenye Uwanja wa Mhangu, Kata ya Salawe, Wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Leo Jumanne Disemba 10, 2024 Mwasenge FC wameonyesha uwezo wa hali ya juu
baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mahando FC, na hivyo
kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali.
Msimamizi wa ligi hiyo, Mwalimu Emmanuel Enock
Kijida, amethibitisha kuwa kesho Salawe FC watakutana na Mwabenda FC katika
mechi ya robo fainali.
“Kwa
matokeo ya leo, Mwasenge FC anasubiri mshindi wa mechi ya kesho ili kukutana
naye katika hatua ya nusu fainali,” amesema Mwalimu
Kijida.
Kwa mujibu wa ratiba, mechi za nusu fainali zitaanza
siku ya Alhamisi, ambapo Beya FC watakutana na Kano FC ambapo Ijumaa itakuwa
zamu ya Mwasenge FC kupambana na mshindi wa mechi ya kesho.
Fainali ya ligi hiyo imepangwa kufanyika Desemba 17, huku mechi ya mshindi wa tatu
ikitarajiwa kuchezwa siku ya Desemba 16.
Mwalimu Kijida ametoa wito kwa wananchi na wadau wa
michezo kufika kwa wingi kushuhudia ligi hiyo ya kipekee, akisema, “Ni fursa
nzuri ya kukuza vipaji vya wachezaji wetu wa Shinyanga na maeneo jirani ikiwa
ni pamoja na kuchochea maendeleo ya michezo.”
Ligi ya Krismas Cup 2024 inadhaminiwa na Makamba
Mussa Lameck kupitia kampuni yake ya MCL inayojihusisha na biashara ya nafaka.
Dhamira kuu ya ligi hiyo ni kuinua vipaji vya michezo na kuchangia maendeleo ya
jamii mkoani Shinyanga.
Msimamizi wa ligi hiyo ya Krismas CUP, Mwalimu
Emmanuel Enock Kijida, akizungumza.
Msimamizi wa ligi hiyo ya Krismas CUP, Mwalimu
Emmanuel Enock Kijida, akizungumza.