Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ndugu Mabala K. Mlolwa amefanya ziara wilayani kishapu Tarehe 12.12.2024. Kunzungumza na wenyeviti wa Serikali za vijiji 117 na wenyeviti wa vitongoji 605.
Lengo la ziara ni kuwapongeza kwa kuchaguliwa na kuwapa Mafunzo ya utendaji kazi ili wakachape kazi vizuri ya kuwatumikia wananchi bila kuwabagua kwa udini, ukabila, ulangi na Wala vyama vyao kwani wote ni Watanzania. Ndugu Mabala, amewakumbusha Wenyeviti kutatua kero za wananchi na kukemea rushwa ili kutowakandamiza wanyonge na aliwaeleza wazi kuwa watakao fanya kinyume na mafunfisho hayo, Chama Cha Mapinduzi hakita mfumbia macho, kitamchukli hatua kali.
Aidha, Mwenyekiti Mabala, amewasisitiza Wenyeviti wa VIJIJI na VITONGOJI kufanya mikutano kwenye maeneo yao ya kuwashukuru wananchi pamoja na kusikiliza changamoto za wananchi na kuzishugulikia, changamoto zilizo juu yao wazipeleka panapo husika ili ziweze kufanyiwa kazi.
Mwisho, ndugu Mabala, amewakumbusha kuendelea kuisemea miradi yote iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania, Maana kila Kijiji na kitongoji kimefikiwa na mradi wa kimaendeleo.
Imetolewa na:-
Ndugu Richard Raphael Masele
Katibu wa Siasa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM,
Mkoa wa Shinyanga