Na Mapuli Kitina Misalaba
Ligi ya Makamba Lameck (Krismas Cup)
inaendelea kwa kasi katika Uwanja wa Mhangu, kata ya Salawe, Wilaya ya
Shinyanga Vijijini, ambapo leo Ikonongo FC imeibuka kidedea kwa kuilaza Mwawile
FC kutoka Misungwi, Mwanza, kwa mabao 5-2.
Msimamizi wa ligi hiyo, Mwalimu Emmanuel
Enock Kijida, amesema ushindi huo umeifanya Ikonongo FC kufuzu kucheza mechi
inayofuata dhidi ya Beya FC, mshindi wa mechi ya jana.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, kesho
kutakuwa na mchezo kati ya Mwagiligili FC na Mahando FC, huku mechi hiyo
ikitanguliwa na mpambano wa mpira wa miguu kwa wasichana kati ya Mhangu
Sekondari na Salawe Sekondari, kuanzia saa 9:00 alasiri.
Mwalimu Kijida amewakaribisha mashabiki wa
soka kujitokeza kwa wingi kushuhudia michezo hiyo, akisema mashindano hayo
yanatoa burudani na kuchochea mshikamano wa kijamii.
Leo ni mechi ya sita katika ligi hii na
kwamba imekuwa kivutio kikubwa kwa maelfu ya wakazi wa Shinyanga na maeneo
jirani.
Mashindano hayo yameandaliwa na Makamba Mussa
Lameck kupitia kampuni yake ya MCL, inayojihusisha na biashara ya nafaka,
yakiwa na lengo la kuibua vipaji vya michezo mkoani Shinyanga.
Mashindano hayo yanatarajiwa kufikia kilele
chake Disemba 17, 2024.
Msimamizi wa ligi ya Krismas CUP, Mwalimu Emmanuel Enock Kijida, akizungumza leo Disemba 4, 2024.
Picha ya pamoja timu ya Ikonongo FC ya kata ya Salawe.Msimamizi wa ligi ya Krismas CUP, Mwalimu
Emmanuel Enock Kijida, akizungumza leo Disemba 4, 2024.
Makamba Mussa Lameck Mkurugenzi wa kampuni ya MCL, inayojihusisha na biashara ya nafaka, ndiye mwandaaji na mdhamini wa ligi ya Krismas CUP inayoendelea kata ya Salawe Wilaya ya Shinyanga Vijijini.
TAZAMA VIDEO