MAKALA: MAFANIKIO (KWA UCHACHE) YA KAZI NA MIRADI ILIYOTEKELEZWA NA MBUNGE WA JIMBO LA SHINYANGA MJINI MHE. PASCHAL PARTOBAS KATAMBI

 

Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Paschal Katambi.

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mhe. Paschal Partobas Katambi, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, amekuwa akitekeleza kwa mafanikio makubwa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025 chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 Katika kipindi cha miaka minne (4), utekelezaji umejikita kwenye maeneo muhimu kama vile elimu, afya, miundombinu ya barabara, maji, masoko, TANESCO, mikopo kwa makundi maalum, walengwa kwa TASAF, kilimo na mifugo pamoja na shughuli za kijamii.

Makala hii inatoa muhtasari wa mafanikio hayo kwa kila sekta.


1. Elimu

Katika sekta ya elimu, Jimbo la Shinyanga Mjini limefanikiwa kuongeza miundombinu na kuboresha huduma za elimu ambapo zaidi ya Bilioni 10 zilitumika kwa kipindi cha miaka minne (4) katika shule za Msingi na Sekondari mpya, kama ifuatavyo:

  • Ujenzi wa shule mpya 9 za msingi na sekondari, ikiwa ni pamoja na:
    • Shule za Sekondari MwangulumbiButengwaLubaga, na Wasichana Shinyanga.
    • Shule za Msingi MwamasheleMwamagulya, Itogwang’olo, Ibadakuli B, na Mwasane.
  • Ujenzi wa vyumba vya madarasa 176 viligharimu Tsh 3.52 bilioni.
  • Ujenzi wa maabara 16 zenye thamani ya Tsh 480 milioni.
  • Ujenzi wa matundu ya vyoo 578 kwenye shule za msingi na sekondari, kwa gharama ya Tsh 1.27 bilioni.
  • Utengenezaji wa madawati 2,379 kwa shule za msingi na 3,125 kwa sekondari.
  • Ujenzi wa mabweni manne kwa sekondari ya Old Shinyanga na bweni la Shule ya Msingi Buhangija.
  • Ukarabati wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Buhangija, pamoja na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo tawi la Shinyanga.
  • Ukarabati wa Chuo cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi (MUCOS), ambao umegharamu Tsh 11.8 bilioni na utaanza muda wowote.

2. Afya

Mbunge Katambi ameendelea kuboresha huduma za afya kwa jamii, ambapo mafanikio ni pamoja na:

  • Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, ambayo imegharimu Tsh 7.3 bilioni.
  • Ununuzi wa magari 6 ya wagonjwa kwa hospitali za Kambarage, Manispaa, Rufaa Negezi, na gari la utawala.
  • Ujenzi wa Hospitali ya Manispaa, ukarabati wa vituo vya afya, na zahanati mpya 6 zilizokamilika.
  • Ukarabati wa Kituo cha Afya Kambarage na zahanati nyingine zenye thamani ya Tsh 500 milioni.
  • Mpango wa kukamilisha zahanati 3 zaidi (Mwamgunguli, Mwagala, Ibinzamata).
  • Manunuzi ya vifaa tiba vya thamani ya Tsh 650 milioni kwa hospitali za Jimbo la Shinyanga Mjini.

3. Barabara

Kwa kipindi cha miaka minne, miundombinu ya barabara imeimarishwa kwa kiasi kikubwa, ambapo Tsh bilioni 5.7 zimetumika kutengeneza barabara za moramu, mitaro, na makalvati. Aidha, jumla ya Tsh 2.5 bilioni zilitolewa kupitia tozo za mfuko wa jimbo kwa ukarabati wa miundombinu.

Mafanikio makubwa ni pamoja na:

  • Ujenzi wa madaraja 8 makubwa na madogo, kama vile Daraja la Uzogore-Bugwandege (Tsh 426 milioni) na Daraja la Ibinzamata-Kitangili (Tsh 200 milioni).
  • Ukarabati wa barabara za lami, zenye urefu wa zaidi ya mita 165 hadi 340, kwa gharama ya Tsh milioni 86 hadi Tsh milioni 183.
  • Ujenzi wa barabara ya lami ya Old Shinyanga-Lubaga (Tsh 710 milioni) na daraja la Ndala-Mwasese.
  • Ujenzi wa kiwanja cha ndege Ibadakuli umefikia asilimia 20, na kazi inaendelea.

4. Maji

Huduma ya maji Jimbo la Shinyanga Mjini imeimarishwa kwa kiasi kikubwa, ambapo:

  • Zaidi ya Tsh 1 bilioni zilitumika katika miradi ya maji.
  • Usambazaji wa maji umefanyika katika maeneo ya Bugwandege, Masekelo, Mwamashele, Mwanubi, Busongo, na maeneo ya mjini.
  • Tsh 195 bilioni zimepangwa kwa usambazaji zaidi wa maji kuanzia mwaka 2024-2025.

5. Masoko

Jimbo la Shinyanga Mjini limefanikiwa kujenga masoko mapya na kuboresha yale ya zamani:

  • Soko kuu limeboreshwa kwa gharama ya Tsh bilioni 1.84.
  • Ujenzi wa masoko ya Ngokolo, Ibinzamata, na Soko la mboga mboga mnara wa voda kwa jumla ya Tsh bilioni 1.31.
  • Ukarabati wa stendi na maeneo ya biashara, ikiwemo Stendi ya Kambarage na Soko la Majengo Mapya.
  • Ujenzi wa Jengo la Utawala la Manispaa umegharimu Tsh bilioni 3 na unaendelea.

6. Mikopo kwa Wanawake, Vijana, na Walemavu

Katika kipindi cha 2020-2024, mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana, na walemavu imeongezeka, ambapo:

  • Mwaka 2020-2021, vikundi 22 vilipatiwa mikopo ya Tsh milioni 278.
  • Mwaka 2021-2022, vikundi 16 vilipatiwa Tsh milioni 282.
  • Jumla ya mikopo imeendelea kuimarika kila mwaka.

7. Walengwa wa TASAF

Mradi wa TASAF umesaidia walengwa kupata huduma bora, ambapo serikali ya jimbo imekuwa ikiendelea kuboresha ustawi wa jamii kwa kutoa ruzuku na huduma muhimu kwa walengwa wa TASAF, ambao ni wazee, walemavu, na familia zisizojiweza.


8. TANESCO

Kwenye sekta ya nishati, miradi ya kusambaza umeme imefanyika katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:

  • Ujenzi wa laini za msongo mkubwa na mdogo, pamoja na ufungaji wa transfoma.
  • Miradi iliyokamilika katika maeneo ya Bugayambelele, Ndembezi, Ibinzamata, Kitangili, na Butengwa kwa gharama ya zaidi ya Tsh 808 milioni.

9. Kilimo na Mifugo

Katika sekta ya kilimo:

  • Usambazaji wa pembejeo za kilimo, mbegu, na viuatilifu kwa wakulima wa pamba.
  • Idadi ya wakulima waliopatiwa mbolea kwa bei ya ruzuku imeongezeka, na vifaa vya kilimo vimeboreshwa.

10. Shughuli za Kijamii

Mhe. Katambi ameshiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii kama vile:

  • Ujenzi wa nyumba za ibada.
  • Kushiriki kwenye misiba, sherehe mbalimbali, na kuimarisha uhusiano mzuri kati ya serikali na wananchi.
  • Amewezesha ujenzi wa Ofisi za Chama cha Mapinduzi mbili katika Kata ya Ibadakuli moja na Kata ya Chibe moja Ofisi hizo zimegharimu Tshs 108,000,000/=

Baadhi ya wananchi wa Shinyanga wanasifu juhudi za Mbunge Mhe. Paschal Partobas Katambi kwa kuboresha hali ya maisha yao kupitia sekta mbalimbali. Wakazi wa maeneo tofauti wameeleza kuridhika na miradi ya maendeleo, hususan katika huduma za afya, elimu, na miundombinu.

"Hali ya maji imekuwa bora zaidi kuliko miaka iliyopita."

 Baadhi ya viongozi wa maeneo hayo pia wamepongeza, wakisisitiza kwamba utekelezaji wa Ilani ya CCM chini ya Rais Samia Suluhu Hassan umekuwa na manufaa makubwa kwa jamii.

Hitimisho

Kwa kipindi cha miaka minne, Mhe. Paschal Partobas Katambi ameonesha juhudi kubwa katika kutekeleza Ilani ya CCM Jimbo la Shinyanga Mjini mafanikio haya yanadhihirisha dhamira ya Mbunge katika kuboresha maisha ya wananchi wa Shinyanga kupitia elimu bora, huduma za afya, miundombinu imara, na fursa za maendeleo ya kiuchumi.

Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Moja ya jengo la shule ya sekondari ya wasichana Shinyanga.






Soko kuu la wafanyabiashara wa Mitumba la Mkoa wa Shinyanga lililopo kata ya Ngokolo.































Previous Post Next Post