MKUTANO MKUU MISA -TAN WAFANYIKA DODOMA

Na Kadama Malunde 

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kulinda heshima ya taaluma yao, akitahadharisha kuhusu ongezeko la watu wasiokuwa na ujuzi wa uandishi wa habari ambao wanatumia mitandao ya kijamii kueneza taarifa zisizo za kweli na za kuchafua jamii.

Akifungua mkutano mkuu wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN) ulioambatana na Mkutano wa Uchaguzi leo Jumatano, Novemba 4, 2024 katika ukumbi wa UCSAF Jijini Dodoma, Shekimweri amesema kuwa hali hii inachangia kuharibu taswira ya waandishi wa habari wa kweli na kuathiri hadhi ya taaluma hiyo.

Akizungumza katika mkutano huo uliotanguliwa na Semina kuhusu Habari Potofu, Shekimweri amesisitiza umuhimu wa weledi na maadili katika tasnia ya habari, ili kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinabaki kuwa chanzo cha taarifa za kuaminika na zinazolinda maslahi ya umma.

"Upo umuhimu mkubwa wa waandishi wa habari kuzingatia miongozo ya kitaaluma na maadili ya uandishi wa habari. Watu wasiokuwa na elimu ya uandishi wa habari wamevamia fani hii na wanachafua taswira ya waandishi wa habari wa kweli. Ni muhimu kuhakikisha kwamba taaluma hii inaheshimiwa na wale wanaofanya kazi hii wanazingatia weledi na maadili",amesema.

Mkuu huyo wa wilaya ameeleza kuwa mitandao ya kijamii, licha ya kutoa fursa ya kutangaza taarifa kwa haraka, inapaswa kutumika kwa ustadi na umakini mkubwa.

Ameongeza kuwa waandishi wa habari wanapaswa kutumia mitandao hii kwa manufaa ya jamii na kwa njia inayolinda amani na usalama wa taifa.

"Tutumie mitandao ya kijamii kwa uangalifu na weledi, na tuwe na jukumu la kuhakikisha kuwa tunalinda amani ya nchi yetu kupitia taarifa tunazozitoa," amesema Shekimweri.

Aidha, Shekimweri amesisitiza kuwa waandishi wa habari wanapaswa kuwa wazalendo na kuhakikisha kwamba maslahi ya taifa yanazingatiwa katika kila taarifa wanayochapisha.

Amewahimiza waandishi wa habari kuwa na jukumu la kutangaza ukweli, huku wakiwajibika kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Mkutano wa MISA TAN ni jukwaa muhimu kwa waandishi wa habari kujadili changamoto zinazokabiliana na sekta ya habari, na kutafuta mikakati bora ya kuboresha uandishi wa habari nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu wa MISA-TAN  leo Jumatano, Novemba 4, 2024 katika ukumbi wa UCSAF Jijini Dodoma 
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu wa MISA-TAN 

Mwenyekiti wa MISA TAN, Salome Kitomari akizungumza kwenye Mkutano mkuu wa MISA-TAN 

Mkurugenzi wa MISA TAN, Elizabeth Riziki akizungumza kwenye Mkutano mkuu wa MISA-TAN 

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri na washiriki wa Mkutano wa MISA TAN wakipiga picha ya pamoja

Previous Post Next Post