MWENYEKITI NYANG'HWALE ATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA KILIMO

Mwenyekit wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Geita Alhaji Adam amewataka vijana kuchangamkia fursa ya kilimo katika kipindi hiki cha mvua Ili kukabili changamoto ya ajira iliyopo nchini. 

Akizungumza Leo 4/12/2024 wilayani ya Nyang'hwale amewataka vijana wilayani humo kulima mazao ya Chakula na Biashara Ili waondokane na changamoto za kiuchumi zinazowakabili.

Adam alisema kilimo ni uti wa mgongo wa taifa letu hivyo ni vyema watanzania kutambua umuhimu wa kilimo kuwa itawasaidia kujikomboa kiuchumi na kuondokana na adha zinazowakabili za ukosefu wa ajira katika eneo lao.

Wakati huohuo Mwenyekiti huyo ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha  wakulima kupata  mbolea na huduma za ughani kuwezesha mapinduzi chanya ya kilimo.












Previous Post Next Post