Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Pwani, Ndugu Ally Hengo, amefariki dunia leo mchana katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es salaam alikokuwa akitibiwa kutokana na majeraha ya ajali aliyoipata.
Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Pwani imethibitisha kifo hicho na inatoa pole kwa familia ya marehemu, wanachama wa klabu hiyo, na waandishi wa habari wote nchini.
Mipango ya maziko inaendelea, na taarifa zaidi zitatolewa.
R.I.P Ally Hengo