Diwani wa Kata ya Old Shinyanga Mheshimiwa Enock Charles Lyeta akizungumza.
Diwani wa Kata ya Old Shinyanga Mheshimiwa Enock Charles Lyeta akizungumza.
Diwani wa Kata ya Old Shinyanga Mheshimiwa Enock Charles Lyeta akizungumza.
Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini Bwana Shabani Athuman Katambi akizungumza.
Diwani wa Kata ya Old Shinyanga Mheshimiwa Enock Charles Lyeta akizungumza.
Diwani wa Kata ya Old Shinyanga Mheshimiwa Enock Charles Lyeta akizungumza.
Diwani wa Kata ya Old Shinyanga Mheshimiwa Enock Charles Lyeta akizungumza.
Na Elisha Petro, Misalaba Media
Diwani wa Kata ya Old Shinyanga Mheshimiwa Enock Charles Lyeta amewataka Vijana ikiwemo waendesha Pikipiki za abiria (Boda boda) kuchangamkia fursa ya mikopo ya Serikali ili kuwekeza katika miradi mbalimbali na kujenga uchumi endelevu.
Ameyasema hayo katika kikao cha Muungano wa Vijana waendesha Pikipiki za abiria (Boda boda) Kata ya Old Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi mpya wa Wangalala na kuwahakikishia upatikanaji wa mikopo hiyo kwa asilimia 100 kwani dirisha la uombaji wa mikopo limefunguliwa.
"Vijana changamkieni fursa ya kupata hii mikopo nafuu kutoka Serikalini kipindi cha nyuma kidogo tulikuwa na mchakato wa kutoa mikopo kwa makundi ya Vijana,akina mama na watu wenye ulemavu lakini Serikali ilisimamisha na kutafuta namna mpya ya kusaidia makundi haya likiwemo kundi lenu vijana na sasa mchakato umekamilika dirisha la utolewaji wa mikopo hiyo limefunguliwa na mikopo hii inatolewa kuanzia umri wa miaka 18-45, Kuna mikopo ya Pikipiki na fedha pia zinatolewa ili kama kuna mradi wowote mnaanzisha mnaweza kukopa fedha na mkafanya mradi wenu kwa hiyo ni jukumu lenu kwa kushirikiana na viongozi wenu kufuata taratibu zote zinazohitajika ili mpate mikopo hiyo"
Katika hatua nyingine Diwani Enock amewasisitiza vijana hao kufanya kazi kwa Umoja,Upendo na Mshikamano ili kufanikisha malengo yao kwa pamoja.
"Tunapaswa kufanya kazi kwa Umoja, Upendo na Mshikamano kwani tukitengana tu haitapendeza, mwenzetu akipata shida tumsaidie kwa pamoja naamini hakuna jambo linaloshindikana lakini ukiwa peke yako unaweza ukashindwa kufanya baadhi ya mambo tuungane ili tufanye mambo makubwa yenye faida kubwa kwetu"
Kwa upande wake Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini Bwana Shabani Athuman Katambi amewaasa Vijana hao kutenganisha muda wa kazi na starehe ili kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
" Wakati mnafanya kazi hakikisheni mnatenganisha muda wa kazi na starehe haswa ulevi ili muweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa na kwa muda mrefu mkichanganya kazi na starehe zingine kama ulevi mtasababisha ajali nyingi kwa hiyo tenganisheni muda wa kazi na starehe"
Kwa upande wao Vijana akiwemo Mwenyekiti wa waendesha Pikipiki za abiria Wilaya ya Shinyanga Mjini Bwana Rivi Maige na Katibu wa waendesha Pikipiki za abiria Kata Old Shinyanga Paschal Juma wameahidi kusimamia vyema maslahi ya Vijana wao na kufanya kazi kwa Umoja,Upendo na Mshikamano ili kufikia malengo waliyojiwekea ya kuwa na uchumi endelevu.