MWENYEKITI SMAUJATA SHINYANGA NABILA KISENDI AWASHAURI WAZAZI KUPELEKA WATOTO KWENYE ELIMU YA AWALI KATIKA KITUO CHA MAKOLO DAY CARE

Na Mwandishi Wetu, Misalaba Media 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga, Bi. Nabila Kisendi, amewahimiza wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kujifunza elimu ya awali kwenye kituo cha Makolo Day Care ili kuwajengea msingi bora wa elimu.

Bi. Kisendi ametoa wito huo wakati akihutubia katika mahafali ya kwanza ya kituo cha Makolo Day Care kilichopo Kolandoto, Manispaa ya Shinyanga, ambapo wahitimu 10 wa kituo hicho waliagwa rasmi kwa ajili ya kuanza darasa la kwanza mwaka 2025.

Akizungumza katika sherehe hiyo, Bi. Kisendi amesema elimu ya awali ni msingi muhimu kwa maendeleo ya mtoto, na wazazi wanapaswa kutambua nafasi yao katika kuhakikisha watoto wanapata fursa hiyo.
Pia amezungumzia swala  la malezi ya watoto ambapo amewahimiza wazazi kuwa makini katika kuwalea watoto katika maadili na misingi bora ya makuzi ya wa wtoto ili kuepukana na ukatili.

Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wachungaji, Mwenyekiti wa SMAUJATA Wilaya ya Kishapu, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Makolo Day Care, pamoja na vikundi vya kwaya kama Evangelical Assemblies of God Tanzania (EAGT) Kolandoto, Baptist Tinde, na New Pentecost Shinyanga vilivyotoa burudani.

Katika hotuba yake, Mkurugenzi wa kituo hicho Bwana Emmanuel Makolo amesisitiza dhamira ya Makolo Day Care ya kuhakikisha watoto wanapata malezi bora kiroho, kijamii, na kielimu.

Wahitimu walikabidhiwa vyeti na zawadi mbalimbali, huku wazazi wakionesha furaha kwa mafanikio ya watoto wao na juhudi za kituo hicho.

Tazama picha mbalimbali 






















 



































































































Previous Post Next Post