PINDA AKOSHWA NA UBUNIFU WA WAHITIMU ARITA AELEKEZA WAPELEKWE WIZARANI

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. Geophrey Mizengo Pinda (Mb.) amepongeza ubunifu wa utafiti wa taarifa za kijiografia uliobuniwa na wahitimu wa chuo cha Ardhi Tabora (ARITA).

Hayo yamesemwa leo tarehe 13 Desemba 2024 katika mahafali ya 42 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika mtaa wa Ikulu katika kata ya Cheyo Mkoani Tabora.

Mhe Pinda ameongeza Kuwa wahitimu hao ambao ni wataalam wa tehama waamdaliwe utaratibu unaofaa ili kuweza kutumia ubunifu wao kusaidia kukuza maendeleo ya sekta ya ardhi nchini.

Aidha mhe. Pinda ametoa wito kwa halmashauri zote nchini kuvitumia vyuo vya Ardhi Tabora na Morogoro katika kupanga matumizi ya Ardhi, kupima viwanja na kuvimilikisha kwani ardhi isiyopimwa na isiyomilikishwa kisheria ni sawa na mtaji mfu.

Katika hatua nyingine mhe. Naibu Waziri Pinda amewaasa wahitimu kutupilia mbali vitendo vya wizi, dhuluma, ubadhilifu, kuomba na kupokea rushwa hivyo watumie ujuzi walioupata chuoni kuleta mamufaa kwa umma wa watanzania ikizingatiwa ardhi ni jukwaa la maendeleo ya kila mtanzania.

Jumla ya wahitimu 1097 wametunukiwa Astashajada na Stashahada katika fani za urasimu ramani, Usimamizi wa Ardhi, Sanaa, Ubunifu na Uchapaji, Usimamizi wa Mazingira na Mifumo ya Tehama.












 



Previous Post Next Post